Beki na nahodha wa zamani wa Manchester United, Gary Neville, amesisitiza kuwa Arsenal lazima waibuke na ushindi dhidi ya Manchester City katika Uwanja wa Etihad iwapo wanataka kuwa mabingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu.

Neville ametoa kauli hiyo baada ya Arsenal kushinda kwa mabao 4-1 dhidi ya Tottenham Hotspur jana Jumapili, Februari, 22, 2026, ushindi uliowawezesha kurekebisha nafasi yao na kuongoza msimamo wa EPL kwa tofauti ya pointi tano mbele ya Man City. Hata hivyo, timu ya Mikel Arteta imeshacheza mechi moja zaidi kuliko Man City.

Baadhi ya wachezaji wa Arsenal katika mechi ya Ligi Kuu England ambayo wameibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Tottenham. Picha na Mtandao

Arsenal inatarajia kukutana na Manchester City katika fainali ya Kombe la Carabao Machi 22, 2026 kabla ya kutifuana ndani ya Ligi Kuu England, Aprili 18, 2026.

Akizungumza kupitia Sky Sports, Neville amesema: “Nimekuwa nikifikiria kwa muda mrefu Arsenal wanapokuwa wakipigania taji hili, lazima waende na kushinda Etihad. Hiyo ndiyo njia pekee halisi.

Kiungo mshambuliaji wa Arsenal, Eberechi Eze akishangilia moja ya bao alilofunga katika ushindi wa 4-1 iliyopata timu yake katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Spurs Jumapili, Februari 22, 2026. Picha na Mtandao

“Fainali ya Carabao Cup (Machi 22, 2026) ni fursa ya kutuma ujumbe, kwa sababu unacheza moja kwa moja dhidi yao, lakini kile unachoweza kufanya kweli ni kwenda na kuwapiga kwenye uwanja wao wenyewe.”

Ushauri wa Neville unasisitiza kuwa Arsenal itahitaji nguvu na mkakati thabiti ili kudhibiti ushindani kutoka kwa mabingwa wa Ligi Kuu, huku mashabiki wakitarajia pambano la ushindani mkubwa katika mechi zijazo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *