
Mshauri wa rais wa Marekani kuhusu masuala ya Afrika na nchi za Kiarabu, Massad Boulos, amezitaka pande hasimu nchini Sudan kukubali mpango wa usitishaji mapigano bila masharti, wakati huu watu zaidi wakiripotiwa kuuawa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hapo jana Wizara ya mambo ya nje ya sudan ilijibu mapendekezo ya amani yaliyowasiloishwa na Boulos, ikisema Sudan haitakubali mapendekezo yoyote yasiyozingatia maslahi ya taifa.
Mwenyekiti wa Baraza la uongozi, Abdel Fattah al-Burhan akizungumza katika hafla moja, alisema hawana suluhisho lingine isipokuwa kuendelea na vita hadi adui atakapojisalimisha.
Kwa upande wake Boulos, amezihiliza pande husika kukubali mara moja usitishaji mapigano bila chini ya usimamizi wa Umoja wa mataifa, ili kutoa nafasi kwa misaada, uokoaji na kupisha mazungumzo ya amani.
Aidha, afisa huyo wa Marekani alibainisha uwepo wa mpango wa kuwawekea vikwazo viongozi wa kundi la RSF, akiwatuhumu kuhusika na mauaji ya kimbari, katika mji wa El-Fasher.