Nchi ya Uganda inataka kuunganisha reli yake inayoendelea kujengwa na ile ya nchi jirani ya Tanzania, mpango unaotarajiwa kurahisisha usafirishaji wa madini kama dhahabu, kulingana na stakabadhi ambazo zimeonekana na shirika la habari la Reuters.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Uganda kwa sasa inasafirisha sehemu kubwa ya bidhaa zake kupitia bandari ya Mombasa nchini Kenya, ikiwa tayari imetangaza nia ya kuunganisha reli yake ya mwendo kasi na ile iliojengwa nchini Kenya, mpango ambao hadi sasa unaendelea kushugulikiwa.

Kulingana na stakabadhi kutoka kwa Wizara ya uchukuzi ya Uganda, reli hiyo itaanzia kwenye mpaka na Tanzania hadi kusini pamoja na kusini Magharibi mwa Uganda na kisha katika Mji wa Mpondwe mpaka na jirani na nchi ya DRC.

Wanafunzi wakiabiri treni nchini Kenya.
Wanafunzi wakiabiri treni nchini Kenya. REUTERS – Baz Ratner

Inaripotiwa kuwa lengo kuu la kuunganisha reli hizo ni kurahisisha usafirishaji wa madini kati ya Uganda na Tanzania kuelekea bandari ya Dar es Salaam pamoja na kupunguza gharama ya sasa ya usafirishaji. 

Mradi huo utafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambao nchi ya DRC itapewa nafasi ya kujiunga na reli hiyo iwapo itataka kufanya hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *