
Rais wa zamani wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol amekata rufaa dhidi ya kifungo chake cha maisha kwa kutangaza sheria ya kijeshi mwaka 2024, mawakili wake wametangaza leo Jumanne.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Tunaamini ni jukumu letu kuonyesha wazi matatizo ya uamuzi huu, si tu katika rekodi za mahakama, bali pia kwa hukumu ya vizazi vijavyo,” timu ya wanasheria ya Yoon imesema katika taarifa.
Siku ya Alhamisi ya wiki iliyopita, Mahakama ya Wilaya ya Kati ya Seoul ilimhukumu Yoon kifungo cha maisha kwa “kuongoza uasi” kwa kutangaza ghafla sheria ya kijeshi mnamo Desemba 3, 2024, na kupeleka jeshi kuzuia bunge kutekeleza majukumu yake.
Kiongozi huyo wa zamani wa kihafidhina mwenye umri wa miaka 65 alihalalisha hatua hii kali kwa kutaja vitisho visivyoeleweka alivyodai vilitolewa na “wale wanaopinga serikali” walio na uhusiano na Korea Kaskazini, na kwamba bunge lililotawaliwa na upinzani lilikuwa likizuia mipango yake yote.
Mahakama iliamua kwamba “nia” ya Bw. Yoon wakati wa mgogoro wa sheria za kijeshi “ilikuwa ni kuzorotesha shughuli za Bungena kulinyamanzisha kwa muda mrefu,” kulingana na Jaji Ji Gwi-yeon.
Idadi ya kutosha ya wabunge waliweza kuingia ndani ya jengo la Bunge, ambalo lilikuwa limezungukwa na wanajeshi, na kupitisha azimio dhidi ya kunyakua madaraka, na kumlazimisha kurudi nyuma.
Serikali ya kiraia hatimaye ilisitishwa kwa saa sita pekee, lakini jaribio hilo lilisababisha mgogoro mkubwa wa kisiasa nchini. Lilisababisha maandamano makubwa, likasababisha hofu katika masoko ya hisa.
“Ingawa uamuzi huu (wa sheria za kijeshi) ulifanywa kwa kile nilichoamini kuwa ni maslahi ya kitaifa, ninaomba radhi kwa dhati kwa watu kwa kuchanganyikiwa na ugumu ambao hatimaye ulitokana na mapungufu yangu,” Bw. Yoon alisema katika taarifa iliyotolewa Ijumaa kupitia wakili wake.
“Hatutakaa kimya dhidi ya mambo mengi yanayomnyima haki”Bw. Yoon, mawakili wake wamesema siku ya Jumanne.