
Ethiopia, siku ya Jumatatu ilmebadilisha mpaka wa uchaguzi wa Tigray, ambapo wengi wanahofia vita vipya vinakuja, katika hatua iliyoshutumiwa kama “tishio la amani” na viongozi wa Tigray.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Tangazo hilo la tume ya uchaguzi lilikuja kabla ya uchaguzi wa shirikisho uliopangwa kufanyika Juni 1.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 2020-2022 kati ya serikali ya shirikisho na waasi wa Tigray viliua watu wasiopungua 600,000.
Kwa kukiuka makubaliano ya amani ya 2022 yaliyomaliza vita, vikosi vinavyoshirikiana na serikali na vinavyotoka katika eneo jirani la Amhara havijawahi kujiondoa kutoka baadhi ya maeneo ya mpaka wa Tigray.
Tume ya uchaguzi ilisema “maeneo matano yenye migogoro” kando ya mpaka yanapaswa kuchukuliwa kama tofauti na Tigray “hadi madai yao yatakapotatuliwa”.
Utawala wa sasa wa Tigray, uliowekwa na serikali ya shirikisho, uliita tangazo hilo “ukiukaji mkubwa wa katiba na Mkataba wa Pretoria”, ukimaanisha makubaliano ya amani ya mwaka 2022.
Getachew Reda, kiongozi wa waasi wa Tigray wakati wa vita ambaye amejiunga na serikali ya shirikisho tangu wakati huo, pia alikosoa tangazo hilo, akisema “litavuruga amani ya nchi yetu”.
Hofu ya migogoro mipya inaongezeka, kwani vikosi vya shirikisho na TPLF vimekuwa vikikusanyika katika mpaka wao katika wiki za hivi karibuni, na kusababisha mapigano mafupi mwezi uliopita.
Kundi la Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) lilitawala Ethiopia kuanzia mwaka 1991 hadi Waziri Mkuu Abiy Ahmed alipoingia madarakani mwaka wa 2018.
Abiy ameitenga TPLF na kuipiga marufuku kabisa mwaka jana. TPLF haina wawakilishi katika bunge la sasa la shirikisho, lililochaguliwa mwaka wa 2021, kwa sababu uchaguzi ulifanyika wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.