Mamlaka nchini Uganda zimeendelea kuwashikilia wanawake wawili waliokamatwa kwa kosa la kubusiana hadharani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wendy faith na Alesi Diana Denise wenye umri wa miaka 22 na 21 mtawalia walikamatwa tarehe 18 mwezi huu wa Februari, baada ya majirani kuwasilisha malalamiko kwa polisi.

Msemaji wa polisi katika mji wa Arua ameiambia AFP kwamba wawili hao walikuwa wakiendeleza mapenzi ya jinsia moja na walionekana wakibusiana hadharani, na kuongeza kuwa majirani walichukua ushahidi wa picha ya wawili hao.

Aidha majirani wamesema kuwa waliwaona wanawake wengi wakiingia kwenye chumba cha kupanga katika tukio ambalo walishuku kuwa ni sherehe za ngono za jinsia moja.

Hata hivyo baadhi ya watetezi wa haki za binadamu wamekosoa hatua ya  kukamatwa kwa wanawake hao, wanayosoema inayonesha hali halishi inayowakumba watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Katika sheria ya Uganda ya 2023 inayopinga ushoga, wahusika watakaopatikana wakiendeleza uhusiano wa jinsia moja kwa hiari wanakabiliwa na adhabu ya hadi kifungo cha maisha jela.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *