Idadi ya watu wanaokabiliwa na hali mbaya ya chakula nchini Somalia, iliongezeka maradufu mwaka uliopita hadi kufikia watu milioni 6 na laki 5, wameonya wataalamu wa umoja wa Mataifa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa watalaam wa Umoja wa Mataifa, watu Milioni 6.5 wanakabiliwa na baa la njaa nchini Somalia.

Idadi hiyo, inawajumuisha watu Milioni 2 ambao wapo katika hali mbaya, na wanahitaji msaada wa haraka wa chakula.

Aidha, watalaam hao wanaonya kuwa, iwapo hatua haitochukuliwa, watoto Milioni 1.84 walio chini ya miaka mitano, wapo katika hatari ya kusumbuliwa na utapiamlo, huku wengine 483,000 wakiwa tayari wanahitaji matibabu ya haraka.

Mkimbizi wa ndani akipokea chakula cha msaada nchini Somalia.
Mkimbizi wa ndani akipokea chakula cha msaada nchini Somalia. REUTERS – Feisal Omar

Hali hii ya uhaba wa chakula, imesababisha na ukame ambao umeendelea kwa kirefu kwa sababu ya ukosefu wa mvua, bei ya vyakula kuongezeka na utovu wa usalama katika maeneo ya Kati, Kusini na baadhi ya Kaskazini mwa Somalia.

Ripoti hii ya wataalam wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na masuala ya usalama wa chakula, inakuja huku Shirika la mpango wa chakula duniani WFP lilionya  kuwa ifikapo mwezi Aprili, huenda ikasitisha utoaji wa misaada ya kibinadamu nchini Somakia iwapo haitapokea msaada mpya wa kifedha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *