
Miezi minne baada ya kuchukua madaraka, Kanali Michaël Randrianirina amepokelewa katika Ikulu ya Élysée siku ya Jumanne, Februari 24, na mwenyeji wake Emmanuel Macron. Wawili hao walichangia chakula cha mchana kilicholenga kurekebisha uhusiano wa pande mbili ulioathiriwa na kuondolewa kwa rais wa zamani Rajoelina wa Madagascar wakati wa kilele cha maandamano dhidi ya utawala wake miezi michache iliyopita.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 3 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mkutano huu huko Paris unakuja huku kukiwa na ushindani mdogo wa kidiplomasia, siku sita tu baada ya ziara ya kiongozi huyo wa Madagascar nchini Urusi abapo alipokelewa katiklu ya Kremlin.
Chakula cha mchana ndio, lakini matokeo ya kisiasa inajidhirisha: Paris na Antananarivo zilifunga mfumo mpya wa ushirikiano kwa miezi 24 ijayo siku ya Jumanne, kulingana na taarifa kutoka Ikulu ya Élysée, anaripoti mwandishi wetu huko Antananarivo, Aurélie Kouman.
“Katika muktadha wa kimataifa uliojaa changamoto nyingi, marais hao wawili walithibitisha tena kujitolea kwao kwa ushirikiano mpya, wenye usawa, na unaoangalia mbele kwa uthabiti, ulioanzishwa kwa heshima ya pande zote na unaolenga matokeo halisi kwa manufaa ya watu wao,” hati hiyo inabainisha.
Kutekeleza mkakati wa mseto wa Madagascar
Viongozi hao wawili “walikubaliana kuhusu mfululizo wa miongozo” inayoweka “njia” ya uhusiano wa pande mbili kwa miaka miwili ijayo, sanjari na mwisho wa mpito uliotangazwa na mamlaka mpya ya Madagascar. Hii inahusisha “kuimarisha uhusiano wa kisiasa,” usaidizi wa Ufaransa kwa “maendeleo ya kiuchumi” ya Madagascar, na “kuendelea na ushirikiano wa usalama na ulinzi.”
Kwa Kanali Michaël Randriarina, suala muhimu lilikuwa kurasimisha mkakati wake wa mseto: “Madagascar haibagui,” alibainisha kabla tu ya ziara yake nchini Ufaransa. Alipokelewa na Vladimir Putin huko Moscow Ijumaa iliyopita.
Lakini ili kurekebisha uhusiano na Ufaransa, ilikuwa muhimu kwanza kutatua masuala yaliyosalia kuhusu hatua ya Paris ya kumtorosha rais wa zamani Andry Rajoelina mwezi Oktoba mwaka uliyopita kufuatia maandamano ya Gen Z, hatua ambayo vijana wa Madagascar wanaiona kama kuingiliwa katika masuala ya ndani ya nchi hiyo.
Siku iliyotangulia, ndege mbili kubwa za mizigo za Urusi zilipeleka tani 60 za msaada wa chakula kwa Antananarivo, moja ya dhihirisho la makubaliano ya kimkakati yaliyosainiwa Kremlin.
Nyanja zinazopewa “kipaumbele” kwa viongozi wa biashara wa Madagascar
Kutokana na mabadiliko haya, Ufaransa inajibu upande wa kiuchumi. Mkutano uliofanyika mara baada ya hapo kati ya viongozi wa biashara wa Madagascar waliopo Paris na shirikisho la waajiri la Ufaransa, MEDEF, ulisababisha mikataba ya ufadhili kwa miradi 29, yenye thamani ya kati ya euro bilioni 1 na euro bilioni 2, haswa katika sekta zinazoitwa “kipaumbele”: utalii, mafunzo, teknolojia ya kidijitali, na haswa nishati.
Nchini Madagascar, kukatika kwa umeme kunaathiri maisha ya kila siku ya kaya na biashara sawa. Kikwazo hiki kikubwa kwa shughuli za kiuchumi hufanya uwekezaji wa nishati kuwa wa dharura. Kwa hivyo, miradi mitano imetambuliwa, ikichanganya nishati ya jua, gridi ndogo zilizogawanywa katika maeneo ya vijijini, na, kwa muda mrefu, mabwawa makubwa ya umeme wa maji, haswa Volobe na Sahofika.
Akihojiwa na Alexis Bedu wa idara ya Uchumi ya RFI, Francis Rabarijohn, rais wa Kundi la Makampuni ya Madagascar, anaelezea kwamba “lazima tuweke kipaumbele miradi yenye matokeo yanayoonekana kwa muda mfupi, ndani ya miezi 0-24, au angalau miezi 0-12.”
Ushirika huu wa Ulaya ni muhimu zaidi kwa Antananarivo kutokana na uhusiano wa kibiashara uliopo. Mwaka jana, ushuru wa hadi 47% uliwekwa kwa bidhaa za Madagascar. Na licha ya kufutwa kwake na Mahakama Kuu ya Marekani, kutokuwa na uhakika bado kunabaki kwa viongozi wa biashara wa Madagascar.
“Hatujui kitakachotokea. Katika mwezi mmoja, katika miezi sita, katika mwaka mmoja. AGOA imeongezwa muda wa mwaka mmoja. Muda huo ni mfupi sana.” “Tulianza kwa 47%, kisha tukashuka hadi 10%, na bado tunasubiri uthibitisho wa takwimu ya 15%. Kuna kutokuwa na uhakika, na hilo linazuia uwekezaji chanya,” analalamika rais wa kundi la makampuni ya Madagascar.
Hili linakuja huku tasnia ya nguo ya Madagaska ikiwa tayari imedhoofika na inakabiliwa na ushindani ulioongezeka, haswa kutoka India.