
Zaidi ya watu bilioni 1 duniani, ambao ni sawa na mtu mzima mmoja kati ya wanne, wanahofia kupoteza ardhi yao au makazi katika kipindi cha miaka mitano ijayo, ripoti mpya ya umoja wa Mataifa imeonesha.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na chakula FAO, pamoja na taasisi ya muungano wa kimataifa wa Ardhi, unasema kiwa ni asilimia 35 pekee ya umiliki wa ardhi umerekodiwa kisheria, ukiwaacha watu wasio na uwezo katika hatari ya kuondolewa kwenye ardhi yao.
Ripoti imebainisha kuwa ukosefu wa usalama wa ardhi kama kichocheo kikubwa cha ukosefu wa usawa, na kuathiri usalama wa chakula, riziki na ustahimilivu wa hali ya hewa.
Aidha ripoti inaonyesha kuwa serikali zinamiliki kihalali takriban asilimia 64 ya ardhi duniani kote, huku zaidi ya robo ikimilikiwa na watu binafsi na karibu asilimia 10 bado haijasajiliwa.
Katika mataifa yaliyoko kusini mwa jangwa la Sahara, ardhi nyingi hushikiliwa chini ya mifumo ya kitamaduni lakini haina utambuzi rasmi, na hivyo kuongeza hatari kwa jamii, hasa wanawake na watu wa kiasili.
Ripoti hiyo inaonya kwamba bila ulinzi imara wa haki za ardhi na sera jumuishi, mamilioni ya watu wataendelea kuathiriwa na uhamishaji, na hivyo kudhoofisha maendeleo endelevu, usalama wa chakula na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.