Iran na Marekani zinakutana leo Alhamisi, Februari 26, kwa ajili ya duru ya tatu ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja nchini Uswisi, yenye lengo la kuvunja mkwamo wa sasa wa “si vita wala amani,” kwa maneno ya rais wa Iran. Lakini saa chache tu kabla ya kuanza kwa majadiliano haya mjini Geneva, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio ametaja “tatizo kubwa,” akiishutumu Tehran kwa kukataa kujadili mpango wake wa makombora ya masafa marefu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Iran na Marekani zinaanza duru ya tatu ya mazungumzo yasiyo rasmi mjini Geneva leo Alhamisi, Februari 26. Jamhuri ya Kiislamu inataka mazungumzo hayo yajikite kwa suala la nyuklia na inadai kuondolewa kwa vikwazo vinavyoathiri uchumi wake.

Chini ya upatanishi wa Oman, duru ya tatu ya mazungumzo kati ya Iran na Marekani inafanyika leo Alhamisi, Februari 26, mjini Geneva.

Licha ya tofauti zao, Iran inasisitiza kwamba makubaliano “ni jambo muhimu,” kulingana na Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi, ambaye anaongoza ujumbe huo kwenye mazungumzo hayo, akitaja “fursa ya kihistoria.” Rais Massoud Pezeshkian, kwa upande wake, alizungumzia “mtazamo mzuri,” akisema alitarajia kutoka katika hali hii ya “si vita wala amani”.

Marekani inawakilishwa na mjumbe Steve Witkoff na mkwe wa rais wa Marekani, Jared Kushner.

Tangu mwezi Januari, Iran na Marekani zimesema ziko wazi kwa mazungumzo lakini pia zimejiandaa kwa hatua za kijeshi, na kuacha hali zote wazi. Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye ametuma kikosi kikubwa cha kijeshi katika Ghuba, anabainisha kwamba anapendelea azimio la kidiplomasia kuliko mzozo huo, lakini siku ya Jumanne, Februari 24, aliishutumu Tehran kwa kuwa na “matamanio mabaya ya nyuklia.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *