Mauaji ya raia kwenye vita vinavyoendelea nchini Sudan, yaliongezeka mara mbili mwaka 2025, ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mwaka 2024.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa, inayoshughulikia haki za binadamu Volker Turk, amesema licha ya mauaji hayo makubwa, maelfu wamepoteza  maisha na hawajatambuliwa huku wengine, wakiwa hawajapatikana.

Turk amesema hali inaendelea kuwa mbaya nchini Sudan na kulaumu pande wote mbili, jeshi na wanamgambo wa RSF ambao wamekuwa wakipigana tangu Aprili mwaka 2023, kwa kukataa kusitisha vita kwa sababu za kibinadamu.

Aidha, ameyashtumu mataifa ya nje kwa kuchochea vita hivyo, kwa kutoa silaha kwa pande zote zinazoendelea kupigana katika vita ambavyo vimesababisha watu zaidi ya Milioni 11 kuyakimbia makwao.

Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, mauaji makubwa yameripotiwa katika mji wa El-Fasher, jimboni Darfur ambako raia wa kawaida walivamiwa wakiwa kambini mwezi Oktoba mwaka uliopita, sawa na kambi ya Zamzam mwezi Aprili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *