
Nchi za Umoja wa Ulaya (EU) zitaweza kutumia fedha za Ulaya kuwawezesha wanawake kutoa mimba zao kwa hiari kote Ulaya, Tume ya Ulaya imetangaza huko Brussels siku ya Alhamisi, Februari 26, kujibu ombi la kutaka ufadhili wa utoaji mimba “salama”.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Brussels, Pierre Benazet
Katika nchi nyingi za Umoja wa Ulaya (EU), utoaji mimba ni desturi iliyoenea. Hata hivyo, bado kuna tatizo kubwa, au hata haiwezekani, katika idadi ndogo ya nchi wanachama.
Ombi la raia linaloitwa “Sauti Yangu, Chaguo Langu” limekusanya saini milioni 1.2 kuomba Umoja wa Ulaya utenge fedha ili kuwasaidia wanawake ambao hawana ufikiaji wa utoaji mimba halali na salama. Mpango huu wa raia ulipokea idhni kutoka kwa Bunge la Ulaya mnamo mwezi Desemba 2025. Ulipokea idhini ya Tume ya Ulaya mnamo Februari 26, 2026. Jibu lilikuwa chanya, lakini halikufikia matarajio ya waombaji.
Tume ya Ulaya ilitoa idhini kwa nchi 27 wanachama kutumia ufadhili kutoka kwa Mfuko wa Jamii wa Ulaya kuwasaidia wanawake wanaotafuta utoaji mimba. Nchi wanachama zitaweza kutumia fedha hizi kwa ajili ya raia wao (wanawake), na pia wale wa nchi zingine za EU.
Kamishna wa Haki za Wanawake, Hadja Lahbib, anaona hili kama hatua muhimu mbele, akibaini kwamba uamuzi huu utawaruhusu wanawake wote wa Ulaya kupata utoaji mimba salama. Hata hivyo, Tume imekubali kwamba Mfuko wa Jamii wa Ulaya, unaopewa euro bilioni 20 kila mwaka, tayari unaunga mkono mipango inayohusiana na afya. Kwa kweli, hii ni mara ya kwanza kwa utoaji mimba kutajwa waziwazi kama unaostahiki.
Jukwaa la “Sauti Yangu, Chaguo Langu” limekaribisha kile kinachochukuliwa kama “kielelezo cha kisiasa,” ingawa hakuna ufadhili mpya uliotengwa na Tume imethibitisha tena kutoegemea upande wowote. Tume ya Ulaya imekumbusha kwamba mamlaka yake ni ndogo katika shughuli zake na nchi wanachama, ikizingatiwa kwamba ufikiaji wa utoaji mimba unapungua nchini Italia na unazuiliwa vikali nchini Poland na Malta.