
DAR ES SALAAM: TAASISI ya Youth Innovation Foundation imewakutanisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali kutokea Dar es salaam wanaosomea kada Sayansi na teknolojia kwa ajili ya bunifu zinazolenga kutatua matatizo katika jamii inayotuzunguka.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es salaam CPA, Deborah Wami Mkurugenzi wa Youth Innovation Foundation wakati alipowakutanisha wanafunzi hao na kusema kuwa wanatafuta ugunduzi mpya uliopo kwenye sayansi na teknolojia na kuwainua wanafunzi hao.

Aidha Debora amesema wamewakusanya wanafunzi hao ili waweze kuwaingiza kwenye pragramu zao kwa kuwasimamia na kukuza miradi na bunifu zao ili ziweze kuwa kubwa huku akisema wanataka kuwa na vijana 500 katika programu zao .
Kwa Upande wake QS.Bundala Robert Mkadiriaji Majengo kutoka AQRB amesema vijana watawezeshwa katika sayansi na teknolojia kwani dunia ya sasa ndivyo inavyotaka na hakuna budi kuendana nayo kwani pia serikali inaendana na mabadiliko hayo.
Nae mwanafunzi aliyeshiriki hafla hiyo Masaka Julius amesema bunifu wanazozionesha zitasaidia kwa baadae hivyo wameiomba serikali iwashike mkono ili ziweze kukua zaidi