People head for cover in Tehran.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

    • Author, Hafsa Khalil
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Marekani na Israel zimefanya mashambulizi ya pamoja dhidi ya Iran.

Rais wa Marekani Donald Trump ameelezea tukio hilo kuwa”operesheni kubwa za kivita” zinazoendelea na kutoa wito kwa vikosi vya serikali ya Iran kuweka chini silaha zao.

Hapo awali, Waziri wa Ulinzi wa Israel alisema Israel imeanzisha “shambulio la tahadhari” dhidi ya Iran, huku milipuko ikisikika kote nchini humo.

Haya yanajiri baada ya wiki kadhaa za vitisho na mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

haya ndio tunayojua kufikia sasa

Ni nini kinafanyika Iran?

Muda mfupi baada ya saa tatu unusu asubuhi (saa za Tehran) sawa na (06:00 GMT), Shirika la Habari la Iran liliripoti milipuko katika mji Mkuu wa Tehran.

Picha zilizoonekana na BBC zinaonyesha moshi ukifuka kwenye uwanja wa Jomhouri mjini na Hassan Abad Square.

Milipuko pia iliripotiwa kusikika katika miji mingine kadhaa kote nchini, ikijumuisha: Isfahan, Qom, Karaj, na Kermanshah. Kiwango cha majeruhi au uharibifu wowote hakijabainika kufikia sasa.

Aanga ya Iran imefungwa tangu mashambulizi Yyalipoanza, Shitika la Habari la Tasnim lilisema.

Trump ameelezea operesheni hiyo kuwa “kubwa na inayoendelea”.

Video kadhaa zilizothibitishwa na BBC Verify zinaonyesha moshi mkubwa ukifuka kote Tehran.

BBC Verify imeweza kufuatilia na kuthibitisha video moja ikionyesha kombora lililivyopiga eneo karibu na Jumba la Ledership, ofisi ya Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei. Video hiyo hata hivyo hainyeshi moja kwa moja ikiwa kombora hilo lililenga jengo hilo moja kwa moja.

Picha nyingine iliyothibitishwa kutoka eneo hilo hilo inaonyesha moshi mweusi ukifuka juu ya majengo ya makazi na maduka madogo yanayouza bidhaa za vyakula. Pia kuna ripoti za mashambulio hayo kushuhudiwa katika maeneo mengine ya Iran.

A map of the cities that have reportedly been struck.

Marekani na Israel zimesema nini ?

Trump aliweka video kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kuthibitisha kuhusika kwa Marekani katika shambulio hilo.

“Muda mfupi uliopita, jeshi la Marekani limeanzisha operesheni kubwa ndani ya Iran ,”alisema.

”Ninasema usiku wa leo kwamba uhuru wenu umekaribia. Endelea kujikinga. Usiondoke nyumbani kwako. Ni hatari sana nje. Mabomu yatarushwa kila mahali.” alisema Rais Trum katika taarifa baada ya kuthibitisha kuanzishwa kwa operesheni kubwa ya kijeshi nchini Iran.

”Tukimaliza, kuangusha serikali yenu. Itakuwa nafasi yenu kuchukua. Labda hii itakuwa nafasi yako pekee kwa vizazi. Kwa miaka mingi mmeomba usaidizi wa Marekani lakini humkuupata. Hakuna rais aliyekuwa tayari kufanya kile ambacho niko tayari kufanya usiku wa leo. Sasa una rais ambaye anakupa unachotaka. Basi hebu tuone jinsi mnavyojibu.” aliendelea kusema Trump.

”Markani inawaunga mkono kwa nguvu nyingi na. Sasa ni wakati wa kuchukua udhibiti wa hatima yanu na kuachilia mustakabali wenye mafanikio na utukufu ambao uko karibu na wewe kufikia.” alisema.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu pia alitoa wito kwa Wairan wote “kupiga moyo konde na kujiokoa dhidi ya dhulma wanazofanyiwa na kukumbatia Iran huru na yenye amani”.

Akimshukuru Trump, alikariri ujumbe wake kwamba Iran “haitaruhusiwa kuwa na silaha za nyuklia ambazo zitaiwezesha kutishia ulimwengu mzima”.

“Hatua yetu ya pamoja itaunda mazingira kwa watu jasiri wa Iran kuchukua hatima yao mikononi mwao.”

Pia aliwashauri raia wa Israel kufuata miongozo kutoka kwa mamlaka.

Hapo awali, waziri wa ulinzi wa Israel alitangaza “hali ya dharura ” kote Israel.

Iran imejibu vipi?

Jeshi la Israel linasema kuwa limetambua makombora yaliyorushwa na Iran kuelekea Israel, likisema linafanya kila iwezalo “kuzuia na kushambulia vitisho ikilazimika kufanya hivyo”.

Milipuko imesikika katika mji wa Haifa na kwingineko nchini Israel, lakini haijabainika kwa sasa ikiwa haya yalikuwa athari au uvamizi.

Huku hayo yakijiri katika eneo hilo, shirika la habari la serikali la Bahrain liliripoti kushambuliwa kwa kambi ya Jeshi la Wanamaji laMarekani, ambalo liko Bahrain, “limeshambuliwa kwa kombora”.

Haya yanajiri baada ya wizara ya mambo ya ndani ya Bahrain kusema ving’ora vya dharura vimepigwa, na kuwataka wakaazi kuwa watulivu na kuelekea sehemu salama iliyo karibu zaidi.

Wizara ya ulinzi ya Qatar ilisema “ilifanikiwa kukabiliana na mashambulizi kadhaa yaliyolenga eneo la nchi hiyo”, vyombo vya habari vya serikali viliripoti, baada ya milipuko kusikika katika mji mkuu wa Doha.

Qatar ni mwenyeji wa kambi ya kijeshi ya Al Udeid, kituo kikubwa zaidi cha kijeshi cha Marekani katika eneo hilo la mashariki ya kati.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imelaani katika taarifa yake “ukiukaji wa wazi” wa anga yake uliofanywa na Iran katika shambulio la kombora.

Taarifa hiyo ilisema kuwa Qatar “inahaki ya kujibu.”

Waisraeli wameonywa dhidi ya mikusanyiko na kuenda shule au kazini kama sio muhimu. Mwongozo huo uitadumishwa hadi Jumatatu 20:00, mamlaka imesema.

Anga ya Israel pia imefungwa kwa ndege za kiraia, kulingana na vyombo vya habari vya Israeli.

Map of Middle East.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *