Wananchi wa Iran wamemiminika mitaani na katika medani mbali mbali kumuomboleza Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, aliyeuawa shahidi katika shambulizi la kigaidi la Marekani na utawala haramu wa Israel.

Mamilioni ya wananchi Waislamu wa Iran wamekusanyika katika miji mbali mbali wakimuomboleza Kiongozi Muadhamu, huku wakitaka taifa hili lilipize kisasi cha jinai hiyo.

Baraza la Mawaziri la Iran limetangaza siku 40 za maombolezo ya kitaifa kufuatia msiba huo mkubwa wa kuondokewa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

Katika taarifa iliyotolewa mapema leo Jumapili, serikali ya Iran imethibitisha kifo cha Kiongozi Muadhamu, ambaye aliuawa shahidi katika mashambulizi ya kigaidi ya Marekani na Israel mapema jana Jumamosi.

Ikiangazia uongozi wa busara wa Ayatullah Khamenei kwa zaidi ya miaka 37, kubeba kwake bendera ya Uislamu kwa ushujaa na imani, na kuongoza kwake Ummah wa Kiislamu dhidi ya ukafiri na uistikbari, taarifa hiyo imemtaja Shahidi Khamenei kama mfano wa kujitolea mhanga na upinzani katika enzi ya kisasa.

Serikali ya Iran imetoa rambirambi kwa Imam wa Zama (AS), taifa tukufu la Iran, Ummah mkubwa wa Kiislamu, na watu wote wenye mawazo huru duniani kwa msiba huu mkubwa.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza siku 40 za maombolezo ya kitaifa na siku 7 za mapumziko ya umma kwa ajili ya kuomuomboleza Kiongozi Muadhamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *