
DODOMA: Waziri wa Maliasili na Utalii, Ashatu Kijaji amesema uwekezaji wa tekinologia ya kutambua makundi ya tembo ili kudhibiti mwingiliano wa makundi ya wanyama na binadamu kutasaidia kupunguza vifo na uharibifu wa mali na mazao ya wananchi.

Hatua hiyo ya waziri imekuja wakati kukiwa na migogoro katika ya wananchi wanaozunguka hifadhi na wanyama na kuamua kuondoa kilio cha wananchi wa vijiji 11 vya Wilaya ya Kondoa wanaosumbuliwa na tembo kwa kuwafunga tembo wawili vifaa kwa ajili ya kusukuma mawimbi.
Amesema hayo leo Februari 28, 2026 wakati akizindua zoezi la kufunga tembo mkanda wa mawasiliano (GPS SATELLITE COLLAR) Kuelekea kilele cha siku ya wanyama pori duniani Machi 03, 2026 katika pori la akiba la Mkungunero lililopo wilayani Kondoo Mkoa wa Dodoma.

Amesema mikanda hiyo inatoa fursa ya uwezo wa kujua makundi ya tembo yalipofika na kudhibiti uelekeo wa tembo na kufuatilia mwenendo wa tembo katika makazi ya watu.
”Tukishajua tunatuma ndege nyuki ambazo zinakwenda kuzirejesha tembo hizi na makundi ya tembo kurejea katika hifadhi yetu na mapori yetu mbalimbali,”amesema Kijaji.