Viongozi wa dunia, wameendelea kutofautiana kuhusu mashambulio yaliyofanywa Iran na nchi za Israel na Marekani, mashambulizi ambayo yamesababisha kifo cha kiongozi wa juu wa kidini kwenye taifa hilo, Ayatollah Ali Khamenei.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Saa chache baada ya Iran kuthibitisha kifo cha Khamenei, viongozi kadhaa wa dunia walijitokeza, baadhi wakipongeza na wengine wakipinga.

Waliopongeza kifo chake ni pamoja na Rais wa Marekani,  Donald Trump na mshirika wake waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ambapo wamesema kifo chake ni ishara ya mabadiliko na mwanzo mzuri kwa raia wa Iran.

Aidha umoja wa Ulaya pamoja na kukosoa operesheni zinazofanywa pamoja na majibu ya Iran dhidi ya majirani zake, umesema kifo cha Ayatollah kinatoa tumaini jipya kwa raia wa nchi hiyo na mustakabali wa ukanda.

Hata hivyo, mauaji yake hayakuzifurahisha baadhi ya nchi ikiwemo Urusi na Uchina, ambazo kupitia kwa rais Vladmir Putin na Xi Jinping, wamelaani operesheni za Marekani na Israel, wakisema hazikubaliki na zimevuka mipaka.

Wakati huu mataifa yenye nguvu yakitofautiana kuhusu mauaji yake, nchi za ghuba ikiwemo, Saudi Arabia, Qatar, Kuwait na Oman, zimekashifu mashambulio ya Iran dhidi ya miundombinu yao, zikisisitiza kuwa zitajibu kulingana na madhara yaliyojitokeza.

Mgogoro huu mpya umezidisha hofu ya kupanuka kwenye êneo la ukanda, hasa wakati huu Tehran ikidai italenga maslahi yote ya Marekani na washirika wao, wakati huu ukiwatuhumu majirani zake kusaidia Israel na Marekani kushambulia nchi yao.

Katika hatua nyingine kiongozi wa kanisa katoliki, Papa Leo wa 14, ametoa wito wa mapigano kusitishwa na kutoa nafasi kwa majadiliano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *