
Kikosi cha Simba kimewasili Uwanja wa New Amaan Complex saa 12:37 jioni tayari kwa mchezo wa Dabi ya Kariakoo utakaopigwa kuanzia saa 2:15 Usiku.
Katika hali ya kushangaza, kikosi hicho kimetumia mlango usio rasmi kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kikitumia mlango wa VIP ambapo ni kinyume na utaratibu.
Bodi ya Ligi wakati inafanya maandalizi ya mchezo huo, iliandaa maeneo maalumu ya wachezaji hao kuingia kwa timu zote mbili, Simba na Yanga kwa kuweka mabango ya wadhamini.
Yanga ilitumia mlango rasmi tofauti na Simba kama walivyoelekezwa.
Kutumia mlango usio rasmi ni kuvuna kanuni ya 17:21 ya Ligi Kuu Bara inayohusu Taratibu za Mchezo, adhabu yake ni faini ya Sh1 milioni.