Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara limeagiza viongozi wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) – BAWACHA, kuripoti tarehe 2 mbele ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, kwa tuhuma za kukaidi amri halali ya Mahakama Kuu na kufanya shughuli za kisiasa kinyume cha sheria.

Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishina Mwandamizi Msaidizi wa Jeshi la Polisi nchini, Pius Lutumo, ametoa kauli hiyo na kuwataka viongozi wa chama hicho pamoja na baraza la wanawake kuzingatia sheria na taratibu za nchi.

Amewataka waandalizi wa kikao cha kujadili na kupanga maadhimisho ya Siku ya Wanawake Machi 8 kufika na kutoa maelezo kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za kisheria pamoja na maamuzi ya Mahakama Kuu yaliyoweka zuio.

Amesema iwapo watahitaji kufanya shughuli zozote za kisiasa, wanapaswa kurejea Mahakama Kuu kwa mwongozo zaidi

Katika hatua nyingine, Kamanda Lutumo ametoa wito kwa watu wanaotumia mitandao ya kijamii kusambaza taarifa zinazoleta taharuki kuhusu madai ya mke wa askari wilayani Bunda kujeruhiwa, akieleza kuwa taarifa hizo si za kweli bali ni uzushi wenye nia ya kupotosha umma.

Ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Mara kupuuza taarifa zenye dhamira mbaya zinazolenga kuondoa amani na utulivu.

#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *