
Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama kwenye wilaya ya Masisi jimboni Kivu Kaskazini, kumesababisha wimbi jipya la raia wanaokimbia makazi yao na kuingia huko Katoyi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hali hiyo imechangiwa na mapigano yanayoendelea kati ya waasi wa M23 na wapiganaji Wazalendo wanaoshirikiana na jeshi la Serikali.
Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, vurugu hizo zilizuka usiku wa Alhamisi wiki iliyopita na kuathiri vijiji kadhaa, vikiwemo Luke, Ngomashi na Bukumbirire, karibu na eneo la kimkakati la uchimbaji madini la Rubaya.
Ripoti za mashirika ya misaada zinaeleza kuwa watu hao waliwasili katika kambi ya Katoyi kati ya Februari 19 na 24, huku shule katika eneo hilo zikitumika kama makazi ya muda.
Mashirika hayo yanasema idadi ya wakimbizi wa ndani imeongezeka kwa takribani asilimia 85, hali inayodhoofisha zaidi juhudi za usambazaji wa misaada kama chakula, dawa na maji safi.
Wakati huo huo, viongozi wa eneo la Masisi wameitaka jumuiya ya kimataifa kuingilia kati ili kukomesha migogoro ya mara kwa mara inayolikumba jimbo la Kivu Kaskazini.