Nchini Burkina Faso,milipuko ilisikika karibu na makaazi ya rais jijini Ouagadougou, mwishoni mwa wiki iliyopita na kuzua wasiwasi wa kuwepo kwa jaribio la kumpindua kiongozi wa jeshi Ibrahim Traore.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Milio hiyo ilizua wasiwasi katika jiji hilo, kabla ya serikali kutoa taarifa na kueleza kuwa, magari sita yaliyokuwa na vilipuzi ndio yaliyolipuka karibu na makaazi ya rais.

Hata hivyo, Ofisi ya rais Traore haijazugumzia tukio hilo, wakati huu, kukiwa na wasiwasi miongoni mwa wakuu wa jeshi kuhusu hali ya usalama nchini humo.

Baada ya tukio hilo, ripoti zinasema kikao cha wakuu wa usalama, kilichokuwa kifanyike jijini Ouagadougou, hakikuendelea kama ilivyopangwa na kuzua maswali kuhusu  hali ya usalama nchini humo.

Haya yanajiri wakati huu, wanajeshi wa Burkina Faso katika wiki za hivi karibuni wakiendelea kukabiliwa na tishio la mashambulio kutoka kwenye makundi ya kijihadi na kuwepo kwa hofu ya baadhi ya wanajeshi kuuawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *