
Rais wa Marekani Donald Trump amechapisha taarifa ya video kwenye jukwaa lakev la Truth Social akisema Marekani “itasababisha pigo kubwa zaidi” kwa utawala wa Iran.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hata hivyo ameonya kuwa “kuna uwezekano wa kutokea vifo vingi zaidi” vya Wamarekani katika vita hivi vinavyoendelea dhidi ya Iran.
Katika mahojiano mengine ya vyombo vya habari yaliyorushwa kwenye mitandao yake ya kijamii, ameonekana akiwaambia watu wa Marekani kwamba wanapaswa kuwa tayari kukubali kwamba baadhi ya wanajeshi wa Marekani watakufa wakati wa mashambulio ya kijeshi yanayoendelea nchii Iran.
Akizungumza na Shirika la Habari la NBC, Rais Trump amesema operesheni dhidi ya Iran ilifanyika kabla ya muda uliopangwa na inaweza kudumu kwa takriban wiki nne, hadi malengo yote ya Marekani yatimizwe.
Hayo yanajiri wakati inaarifiwa kwamba wanajeshi watatu wa Marekani wameuawa katika vita hivyo na wengine watano wamejeruhiwa.
Amevitaka vikosi vya Iran vya Revolutionary Guard kujisalimisha au wakabiliane na kifo ambacho alionya kuwa kinaweza kisiwe kizuri.