
Mashambulio ya kijeshi nchini Iran, yaliyotekelezwa na jeshi la Marekani na Israel, yamesababisha vifo vya wanafunzi 165 baada ya kushambuliwa kwa shule yao, Kusini mwa Iran.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Shule ya Shajareh Tayyebeh iliyopo katika mji wa Minab, ambayo ni makaazi ya kambi ya jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Iran,ililengwa katika mashambulio hayo, Jumamosi iliyopita.
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, ametuma salamu za pole kwa wale wote walioathiriwa na shambulio hilo, alilosema sio la kibinadamu na ni uvamizi wa nchi yake.
Pezeshkian, ametoa wito kwa watoa huduma, wakiwemo mashirika ya kibinadamu kuwasaidia wanaojeruhiwa katika shambulio hilo.