Waliopora ardhi wapewa wiki mojaWaliopora ardhi wapewa wiki moja

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewapa muda wa wiki moja watu wote waliopora au kutapeli ardhi na mali za wananchi kuzirejesha mara moja, akionya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaokaidi agizo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Chalamila amesema  kumekuwepo na wimbi la migogoro ya ardhi linalosababisha malalamiko na kilio kwa wananchi, hivyo Serikali imelazimika kuchukua hatua za haraka kulidhibiti.

Amesema ndani ya muda huo wa wiki moja, kila aliyehusika na uporaji au utapeli wa mali za wananchi anatakiwa kuhakikisha anazirejesha mara moja. “Nimewapa muda mfupi kurejesha mali zote zilizochukuliwa kinyemela. Ndani ya wiki moja, kila aliyehusika ahakikishe anarudisha mali hizo,” alisema Chalamila.

Ameongeza kuwa baada ya kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ya jiji, tayari maeneo zaidi ya 16 yamerudishwa kwa siri na wahusika, huku Serikali ikiamua kuwasamehe waliorejesha mali hizo kwa hiari bila kushinikizwa. Chalamila ametaja baadhi ya maeneo yanayoongoza kwa malalamiko ya utapeli wa ardhi kuwa ni Kigamboni, Ilala na maeneo mengine ya jiji.

Amesema ofisi yake imepokea malalamiko mengi yanayohusu uporaji wa viwanja, ubadilishaji holela wa umiliki wa ardhi pamoja na mikataba kandamizi ya mikopo inayosababisha wananchi kupoteza mali zao. SOMA: Chalamila asisitiza amani, umoja kwa wakazi wa Dar

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *