Makuhani wa Kiyahudi wanaopinga utawala ghasibu wa Israel wamelaani vita na mashambulizi yanayoendelea kufanywa na utawala haramu wa Israel na Marekani dhidi ya Iran.

Katika taarifa yao ya pamoja, makuhani hao wamesema: Tumekusanyika hapa leo tukiwa watu wenye mitazamo na mielekeo tofauti ili kulaani mashambulizi ya utawala wa Kizayuni. Ni jambo ya kutia aibu!“Haya ni mashambulizi ambayo yanafanyika bila sababu ya maana ambamo idadi kubwa ya raia wasio na hatia, wakiwemo wanawake na watoto wadogo, wanauawa na miondombinu ya kiraia inaharibiwa,” wamesema makuhani hao. Taarifa hii ya makuhani wa Kiyahudi inafuata miito inayoendelea kutolewa na asasi na jumuiya nyingi za kimataifa zinazolaani mashambulizi ya kinyama yaliyoanzishwa na Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *