
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limesisitiza kuwa, wahalifu wa Kimarekani na Kizayuni wajue kwamba hakuna hata moja kati ya jinai na mauaji ya kidhulma wanayofanya yatakayopita bila ya jibu.
Taarifa Nambari 15 iliyotolewa na Idara ya Uhusiano wa Umma ya IRGC imeeleza hayo kuhusiana na jinai zilizofanywa katika muda huu wa siku nne na Marekani na utawala wa kizayuni imeeleza kwamba, vita dhidi ya Marekani na utawala ghasibu vitaendelezwa katika upeo na kina kikubwa zaidi.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa, kinyume na madai na propaganda za uwongo yanayozotoa za kushambulia na kuharibu vituo vya kijeshi vya Iran, katika muda huu wa siku nne, majeshi ya watenda jinai ya Marekani na utawala wa kizayuni yamefanya mlolongo wa mashambulizi ya kiwoga dhidi ya skuli, hospitali, viwanja vya michezo, mikahawa na kumbi za sherehe za harusi kwa lengo la kuzusha hofu na mshtuko kwa umma; mashambulizi ambayo yamepelekea kuuawa shahidi zaidi ya raia madhulumu 700 wa Iran na kujeruhiwa wengine kadhaa.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, kuna ulazima kwa jamii ya kimataifa na taasisi za haki za binadamu kuvunja kimya chao kuhusiana na jinai hizo za kinyama ya raia na kuchukua hatua za kufungulia mashtaka na kuwaadhibu watenda jinai za kizayuni na kimarekani…/