.

Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock

Jeshi la Ulinzi la Israel linasema kuwa limeanza
wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya Iran.

“IDF imeanza mashambulizi yanayolenga
maeneo ya kufyatulia makombora ya utawala wa kigaidi wa Iran, mifumo ya ulinzi
wa anga na miundombinu ya ziada,” Jeshi la Ulinzi la Israeli liliandika
kwenye mtandao wa wa kijamii wa Telegram.

Huku hayo yakijiri Jeshi la Marekani
limewatambua wanajeshi wanne wa kwanza wa Kimarekani waliouawa katika mashambulizi
ya Iran.

Wanajeshi hao wa Akiba wa
Jeshi la Marekani, kutoka Kamandi ya 103 ya Ulinzi ya Des Moines, Iowa, ni pamajo
na:

  • Kapteni Cody A. Khork,
    35, wa Winter Haven, Florida
  • Sajenti Daraja la kwanza
    Noah L. Tietjens, 42, wa Bellevue, Nebraska
  • Sajenti wa Daraja la kwanza
    Nicole M. Amor, 39, wa White Bear Lake, Minnesota
  • Sajenti Declan J. Coady,
    20, wa West Des Moines, Iowa

Wengine wawili waliuawa
katika shambulizi la Iran dhidi ya kituo cha kijeshi huko Kuwait siku ya
Jumapili, lakini bado hawajatambuliwa.

Siku ya Jumatatu Waziri
wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth alisema kwamba ngome ya kijeshi ya Marekani
huko Kuwait ilipigwa wakati shambulio la kulipiza kisasi lililofanywa na Iran.

Vifo hivyo sita pekee ndivyo
vilivyothibitishwa na jeshi la Marekani tangu lilipoanzisha mashambulizi dhidi
ya Iran kwa ushikiano na Israel.

Unaweza kusoma:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *