
Baada ya Wizara ya Fedha nchini Marekani, kuliwekea vikwazo jeshi la Rwanda na maafisa wake wanne waandamamizi kwa sababu ya vita vinavyoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo na kukiuka mkataba wa amani, je vikwazo hivyo vitakuwa na athari gani?
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Baada ya vikwazo hivyo, maswali yameibuka, nini kitafuata? Je, vitashawishi kurejelewa tena kwa michakato ya Washington na Doha? Kwa mujibu wa wachambuzi wanasema muda ndio utakaoamua.
Hii sio mara ya kwanza kwa Rwanda kuwekewa vikwazo kwa sababu ya vita Mashariki mwa DRC, tangu kuchipuka tena kwa waasi wa AFC/M23 w mwaka 2022.
Septemba mwaka 2023, Rwanda iliwekwa kwenye orodha ya nchi zinazotumia silaha kwa watoto kupigana vita.
Februari mwaka 2025, aliyekuwa Mkuu wa majeshi ya Rwanda James Kabarebe, na mshirika wa karibu wa rais Paul Kagame, pia aliwekewa vikwazo.
Hata hivyo, Rwanda inakataa vikwazo hivyo, inavyosema vinaegema upande mmoja. Kigali inashtumu Kinshasa kwa kuendelea kuwaunga mkono waasi wa FDLR ambao wanatishia usalama wa Rwanda.