Nchi za Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, zimekubaliana kuunda kikosi kipya cha wanajeshi 2,000 kwa lengo la kukabiliana na tishio linaloongezeka la makundi ya wanajihadi katika ukanda huo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mpango huo umekuwa ukijadiliwa kwa miaka kadhaa na nchi wanachama 12 wa jumuiya hiyo, hasa kufuatia kuongezeka kwa mashambulizi ya kigaidi katika eneo la Sahel.

Kwa mujibu wa wakuu wa kijeshi wa ukanda huo, kikosi hicho cha wanajeshi 2,000 kiko tayari kuanza operesheni zake wakati wowote, hasa katika kipindi hiki ambacho mashambulizi yanaongezeka.

Kikosi hicho kitasalia katika nchi zao za asili, huku Sierra Leone ikitarajiwa kuwa kituo kikuu cha vifaa na uratibu wa operesheni.

Hata hivyo, maafisa wa jumuiya hiyo bado hawajaweka wazi mpango wa ufadhili wa kikosi hicho kipya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *