Kiongozi wa kiroho wa Iran Ayatollah Ali Khamenei atazikwa katika Mji Mtakatifu wa Mashhad, limeripoti shirika la habari la Fars la nchini Iran.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Khamenei 86, ambaye aliongoza Iran kwa miaka 36 aliuuawa katika mashambulio ya Marekani na Israel nchini humo Jumamosi ya wiki iliopita.
Kabla ya mazishi yake, kutafanyika ibaada kubwa ya kumuaga jijini Tehran kulingana na taarifa ya kikosi cha mapinduzi cha wanajeshi wa Iran.
Alikuwa anatokea katika Mji wa Mashhad, Mji wa pili kwa ukubwa nchini Iran, Mji ambapo baba yake alizikwa katika makaburi ya Imam Reza.
Licha ya kutangaza kwamba atazikwa katika Mji wa Mashhad, Iran haijaweka wazi ni tarehe ipi atazikwa.
Baada ya kifo cha Khamenei, jopo la watu watatu liliteuliwa hadi pale wataalamu wa bunge watakapomteuwa mrithi wake.
Vyombo vya habari vya Iran vimeripoti kwamba mashambulio ya Iran na Israeli yalilenga jengo lililotumiwa na viongozi wa Baraza la Kiroho katika Mji wa Qom Kusini wa Tehran.