Marekani “imeidhinisha” wafanyakazi wake wasio wa lazima kwenye balozi zake Saudi Arabia na Oman kuondoka katika nchi hizo, balozi za nchi hizo mbili za Ghuba zimetangaza siku ya Jumanne. Nchi hizi zimekuwa zikilengwa na mashambulizi ya anga ya Tehran kujibu operesheni ya kijeshi kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani “imeidhinisha wafanyakazi wa serikali wasio wa lazima” na familia zao “kuondoka” Saudi Arabia na Oman kutokana na hatari za kiusalama, balozi hizo zilisema kwenye tovuti zao.

Oman, ambayo ilichukua jukumu la upatanishi katika mazungumzo ya hivi karibuni kati ya Washington na Tehran, ilitoa wito wa kusitisha mapigano, huku Saudi Arabia ikilaani mashambulizi ya Iran, ikiwa ni pamoja na yale dhidi ya ubalozi wa Marekani huko Riyadh.

Saudi Arabia inasema imezuia ndege zisizo na rubani tisa katika anga yake

Wizara ya Ulinzi ya Saudi Arabia imetangaza leo Jumatano asubuhi kuzuia makombora mawili na ndege zisizo na rubani tisa katika anga ya nchi hiyo, katika ujumbe tofauti. “Makombora mawili ya Cruise ya kupambana na meli yalizuiliwa na kuharibiwa huko Kharj,” eneo lililo katikati mwa Saudi Arabia, msemaji wa Wizara ya Ulinzi amesema.

“Ndege zisizo na rubani tisa zilizuiwa na kuharibiwa mara tu baada ya kuingia katika anga yaSaudi Arabia,” alisema mapema kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *