
Rais wa Marekani Donald Trump, siku ya Jumanne, Machi 3, ametishia “kusitisha biashara yoyote na Uhispania,” akikosoa kukataa kwake kuruhusu Marekani kutumiakambi za kijeshi huko Andalusia kwa vita vyake dhidi ya Iran na matumizi yake ya kijeshi, ambayo anaona hayatoshi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ili kuunga mkono shughuli zake nchini Iran, jeshi lilitaka kutumia kambi mbili za Marekani zilizoko Andalusia. Uhispania ilisema “hapana”, na Donald Trump hakufurahishwa hata kidogo na uamuzi huo wa Uhispania, anaripoti mwandishi wetu huko Washington, Vincent Souriau.
“Uhispania ilituambia hatuwezi kutumia kambi zao. Si rafiki mzuri. Uhispania haijaonyesha ushirikiano wowote. Kama unavyojua, ni nchi pekee ya NATO ambayo haitaongeza bajeti yake ya ulinzi kwa 5%. Kwa hivyo tutasitisha biashara yoyote na Uhispania. Hatutaki uhusiano wowote zaidi na Uhispania,” rais wa Marekani ametangaza.
Hapo awali, Friedrich Merz alibaki kimya. Kisha, mwandishi wa habari alipomuuliza, “Donald Trump anafikiria kuiadhibu Uhispania, ungefanya nini?”, Kansela wa Ujerumani alichagua kujibu tu kuhusu NATO na kuepuka kuzua mvutano katika Ofisi ya Oval ya Xhite House. “Tunajaribu kuwashawishi kueleza kwamba ni sehemu ya usalama wetu wa pamoja na kwamba sote lazima tuzingatie takwimu hizi: 3.5% kwa ulinzi na 1.5% kwa miundombinu ya kijeshi. Na Uhispania lazima izingatie hili,” Kansela wa Ujerumani alisema. Alipoondoka kwenye mkutano huo, Friedrich Merz alisema kwamba ana uhakika kwamba Marekani inaiheshimu Ujerumani na ingedumisha uwepo wake wa kijeshi katika ardhi ya Ujerumani.
Serikali ya Uhispania inajibu
Katika taarifa, serikali ya Uhispania imejibu matamshi ya rais wa Marekani, ikidai kwamba Uhispania ni “mshirika wa biashara anayetegemeka kwa nchi 195 duniani kote,” ikiwemo Marekani. “Ikiwa utawala wa Marekani unataka kupitia (uhusiano wake wa kibiashara na Uhispania), lazima ufanye hivyo kwa kuheshimu uhuru wa makampuni binafsi, sheria za kimataifa, na makubaliano ya pande mbili kati ya Umoja wa Ulaya (EU) na Marekani,” Uhispani imesema katika taarifa.
“Nchi yetu ina rasilimali zinazohitajika kudhibiti athari zozote zinazowezekana, kusaidia sekta zinazoweza kuathiriwa, na kubadilisha minyororo ya usambazaji,” pia imesema.
Mapema siku hiyo, kabla ya matamshi ya Donald Trump kuhusu nchi yake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania José Manuel Albares alisema kwamba “hakuwa na mazungumzo na mwakilishi yeyote wa Amerika Kaskazini” wala “hakupokea malalamiko yoyote” kuhusu kambi za kijeshi za Rota na Morón. Alibainisha kwamba kambi hizi, zinazotumika “pamoja na Marekani,” ziko”chini ya uhuru wa Uhispania.”