Kiongozi wa chama cha Democrat katika Bunge la Seneti ya Marekani, Hakeem Jeffries, amekemea kwa ukali serikali ya Donald Trump baada ya shambulizi la kijeshi dhidi ya Iran, akisisitiza kuwa hakuna “tishio tarajiwa” kutoka Iran dhidi ya Marekani.

Kulingana na taarifa za IRNA, Hakeem Jeffries aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu kwamba:  “Nilishiriki katika mkutano wa ufafanuzi wa siri. Hakuna ushahidi wowote unaoonyesh kwamba Marekani ilikuwa chini ya tishio la shambulizi la karibu kutoka Iran. Hakuna ushahidi kuhusiana na hilo.”

Jeffries amesema hatua ya serikali ya Trump dhidi ya Iran ni kinyume cha sheria na ameongeza kuwa Bunge  halikuruhusu shambulio hilo, na Katiba ya Marekani si kitu kinachoweza kushindwa au kupuuzwa.

Ameongeza kuwa wanachama wa chama cha Democrat  watajadili kura inayofuata kuhusu mamlaka ya Trump inayohusu vita dhidi ya Iran.

Hayo yanajiri huku kukishuhudiwa maandamano makubwa maeneo mbali mbali ya Marekani kulaani  mashambulizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Juzu katika jiji la New York wapinzani wa vita na sera za Donald Trump walishiriki katika  maandamano maandamano makubwa katika Medani ya Columbus wakitangaza upinzani wao dhidi ya uchokozi na mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *