
Walinzi wa Mapinduzi wa Iran wametangaza leo Jumapili kwamba wako na uwezo wa kuhimili “angalau miezi sita ya vita vikali” dhidi ya Marekani na Israel. Wanadai kuwa tayari wameshambulia zaidi ya malengo 200 ya Marekani na Israel katika eneo hilo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mamlaka ya Iran imesema inatumai mkutano wa kumteua Kiongozi Mkuu mpya “ndani ya saa 24.” Hossein Mozafari, mjumbe wa Baraza la Wataalamu aliyenukuliwa na shirika la habari la FARS, ametoa wito kwa watu “kujiepusha na uvumi wote na kuenea kwa uvumi kuhusu jambo hili.” Baraza hili la Wataalamu lenye wanachama 88 litamchagua mrithi wa Ali Khamenei. Israel tayari imeonya kwamba kiongozi huyo mpya atalengwa na kuhakikisha anauawa.
Wakati huo huo Donald Trump amesema “lazima ashiriki” katika uteuzi wa mrithi wa Ali Khamenei, aliyeuawa katika shambulio la Jumamosi, na akasema kwamba hakupinga kuwekwa kwa kiongozi mpya wa kidini. Hata hivyo, hakutakuwa na mazungumzo hadi “Iran kabla ya Iran kuwa si tihio kwa Marekani na malengo ya Operesheni Epic Fury yametimizwa,” Ikulu ya White House imetangaza. Siku ya Jumamosi, Machi 7, rais wa Marekani alitaja uwezekano wa kupelekwa kwa wanajeshi wa ardhini nchini Iran katika siku zijazo ili kufuatilia akiba ya uraniunm iliyorutubishwa.
Tangu Jumamosi, Februari 28, Israel na Marekani zimeendelea kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya mji mkuu wa Iran, Tehran.
Kulingana na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, angalau watu 1,332 wameuawa nchini Iran tangu kuanza kwa uhasama, wakiwemo wasichana 175 wa shule na wafanyakazi wa shule katika shambulio dhidi ya shule ya wasichana huko Mina, kusini mwa nchi. Idadi hiyo, ambayo haikuweza kuthibitishwa, labda haijumuishi vifo vya kijeshi vya Walinzi wa Mapinduzi.