Raia wa Iran wanajiandaa hivi leo kumzika kiongozi wao Ali Khamenei katika mji alikozaliwa wa Mashhad ulioko kaskazini mwa Iran, shughuli inayoenda kufanyika wakati huu mashambulizi ya Marekani yakitishia kurejea upya kwa vita kwenye eneo la mashariki ya Kati.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Maziko ya Khamenei, yanafuatia siku kadhaa za jeneza lake kupita katika miji mbalimbali ikiwemo nchini Iraq, ambapo raia walipata nafasi ya kufanya ibada na kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi wao.

Hata hivyo wakati shughuli za mazishi zikielekea ukingoni, Marekani ilianzisha mashambulizi mapya nchini Iran yakiwa ni kujibu kile Washington inasema Tehran kushambulia meli zake kwenye bahari ya Hormuz.

Rais wa Marekani Donald Trump ambaye hapo jana alisema makubaliano ya nchi yake na Iran ya kusitisha mapigano yamekoma rasmi, alionya kuhusu majeshi yake kutekeleza mashambulizi makubwa zaidi dhidi ya Iran ikiwa taifa hilo litaendelea na inachokifanya huko Hormuz.

Waombolezaji wakiwa wamekusanyika siku ya mazishi ya Ayatollah Ali Khamenei aliyekuwa kiongozi wa kiroho wa Iran.
Waombolezaji wakiwa wamekusanyika siku ya mazishi ya Ayatollah Ali Khamenei aliyekuwa kiongozi wa kiroho wa Iran. via REUTERS – Majid Asgaripour

Khamenei ambaye aliuawa katika mashambulio ya Februari 28, ambayo ilikuwa siku ya kwanza ya operesheni za kijeshi za pamoja kati ya Marekani na mshirika wake Israel, mashambulio yaliyoanzisha vita rasmi.

Kufuatia safari ya miji mitakatifu ya Najaf na KKarbala nchini Iraq hapo jana, mwili wake ulitarajiwa kuwasili hivi leo kwenye mji wa Mashhad.

Wadadisi wa mambo wamekuwa wakifuatilia kwa karibu sherehe za mazishi ya Khamenei, kujaribu kuona ikiwa mtoto na mrithi wake Mojtaba Khamenei atahudhuria mazishi yake, Mojtaba pia alijeruhiwa katika mashambulizi yaliyomuua baba yake.

Ali Khamanei aliuawa katika mashambulio ya Israeli na Marekani mwezi Februari tarehe 28 mwaka wa 2026.
Ali Khamanei aliuawa katika mashambulio ya Israeli na Marekani mwezi Februari tarehe 28 mwaka wa 2026. REUTERS – Alkis Konstantinidis

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran, IRNA, Khamenei anatarajiwa kuzikwa Alhamisi jioni katika msikiti wa Imam Reza, msikiti ambao ni maarufu kwa ibada.

Khamenei atazikwa pamoja na mjukuu wake aliyekuwa mchanga wakati wa mashambulizi, mkwe wake, mtoto wake wakike na mke wa Mojtaba Khamenei, Zahra Haddad Adel, ambao wote waliuawa katika mashambulio ya Februari 28.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *