Akizungumza na waandishi wa habari mjini Beirut baada ya wiki mbili za uharibifu mkubwa uliozuka kutokana na mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, António Guterres amebainisha kuwa moto wa maroketi ya Hezbollah kuelekea Israel kwa msaada wa Tehran ulifuatiwa na kampeni ya mabomu ya Israeli iliyo “ya uharibifu mkubwa sana” ambayo inafanya sehemu kubwa za Lebanon “kusiwezekane kuishi humo.”
Vita hii si ya hiari kwa Walebanon
“Watu wa Lebanon hawakuchagua vita hii. Waliibebwa ndani yake,” ameendelea kusema Guterres.
“Vita lazima visitishwe,” amesema kiongozi wa Umoja wa Mataifa, akisisitiza kuwa hakuna suluhisho la kijeshi kwa mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati, bali suluhisho la kidiplomasia kulingana na Katiba ya Umoja wa Mataifa.
Ametambua athari kwa pande zote za Mstari wa Bluu unaotenganisha kusini mwa Lebanon na kaskazini mwa Israel, ambao unashikiliwa na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL chini ya azimio la Baraza la Usalama.
Waisraeli wamerudi kwenye kimbilio kutokana na maroketi ya Hezbollah, huku mamia ya Walebanon wakiuwawa “wakiwemo watoto wengi.”
Zaidi ya watu 800,000 wameazimika kuondoka kutoka makazi yao katika eneo la mzozo kusini mwa nchi hiyo na sehemu zinazolengwa katika kisiwa kinachodhibitiwa na Hezbollah kusini mwa Beirut, kufuatia amri za uhamisho wa watu zilizotolewa na Israeli.
Nimekuja kushikamana na watu wa Lebanon
Wakati wa ziara yake mjini Beirut nchini hii leo Jumamosi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa onyo kali kuhusu mzozo unaoendelea nchini Lebanon, akihimiza pande zote kusitisha mapigano na kurudi kwenye diplomasia.
Katibu Mkuu amesema “Nimekuja na ujumbe kwa wananchi wa Lebanon, kwa pande zinazopigana, na kwa dunia nzima,” akisisitiza kuwa ziara yake imekuwa ishara ya mshikamano na raia walioko kwenye mgogoro.
“Ninaumia moyoni mwangu kuona kipindi hiki kikiwa kimeghubikwa na vurugu zinazoongezeka,” amesema, akibainisha kuwa mapigano haya yanaendelea wakati wa sikukuu za kidini za Ramadan na Kwaresma wakati ambao kwa kawaida huashiria huruma na maisha ya pamoja nchini humo.
Raia wanalipa gharama kubwa zaidi ya mzozo huu
Katibu Mkuu ameelezea hali ya kibinadamu inayozidi kuwa mbaya baada ya mashambulizi ya pande zote kati ya Hezbollah na Israel.
Maroketi na na ndege zisozo na rubani au droni zilizorushwa kuelekea kaskazini mwa Israel na eneo la Golan ya Syria inayokaliwa ziliambatana na mashambulizi ya anga ya Israeli na amri za uhamisho mkubwa wa watu kote Lebanon.
“Mamia ya Walebanon wameuawa, wakiwemo watoto wengi,” amesema, akiongeza kuwa “mamia ya maelfu ya raia wanakimbia bila kitu zaidi ya kile wanachoweza kubeba.”
Baada ya kutembelea aneo ambalo ni kimbilio la familia zilizokimbia makazi yao Beirut, Guterres amesema ushuhuda wao umeonesha gharama ya kibinadamu ya vita. “Kusini kuna hatari ya kubadilika kuwa jangwani,” ameonya, huku sehemu za kusini mwa Beirut zikikabiliwa na hatari ya “kushambuliwa hadi kutoweka kabisa.”
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (katikati), Nawaf Salam Waziri Mkuu wa Lebanon (kulia) wakati wa uzinduzi wa ombi la msaada kwa ajili ya Lebanon.
Diplomasia ndio njia pekee
Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa kuendelea kwa mapigano ya kijeshi kutaongeza mateso pande zote za mpaka.
“Simamisheni mapigano. Simamishe mashambulizi,” amesema kwa msisitizo akiongeza kuwa “Hakuna suluhisho la kijeshi kuna diplomasia, mazungumzo na utekelezaji kamili wa Katiba ya Umoja wa Mataifa na azimio la Baraza la Usalama.”
Guterres amesisitiza kazi ya Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Lebanon, Jeanine Hennis-Plasschaert, anayeshirikiana na wadau wa kikanda na kimataifa kufanikisha kupunguza mvutano na kuanzisha upya mazungumzo. Amekumbusha kuwa kusitishwa kwa mapigano mwishoni mwa 2024 kulitoa fursa ya maendeleo ya kisiasa, lakini hayakukutimizwa kutokana na ukiukaji wa mara kwa mara wa makubaliano.
Walindaamani wako hatarini
Katibu Mkuu pia ametoa heshima kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa waliopo kwenye Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani Lebanon (UNIFIL), walioko kwenye Mstari wa Bluu unaotenganisha Lebanon na Israel. Ameeleza kuwa walinda amani watatu kutoka kikosi cha Ghana walijeruhiwa wakati wa mapigano makali wiki iliyopita, mmoja akijeruhiwa vibaya. “Mashambulizi dhidi ya walinda amani na vituo vyao hayakubaliki kabisa na lazima yakome,” amesema, akionya kuwa matukio kama haya yanaweza kuwa uhalifu wa kivita chini ya sheria za kimataifa.
Guterres pia amesisitiza kuwa raia na miundombinu ya kiraia lazima iheshimiwe na kulindwa kila wakati.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametembelea hema la mkimbizi wa Syria nchini Lebanon
Wito kwa jumuiya ya kimataifa
Akitazama zaidi ya mgogoro wa sasa, Guterres ameitaka jumuiya ya kimataifa kuingilia kati zaidi ili kuimarisha Lebanon na kuunga mkono taasisi zake, hasa Jeshi la Wanamaji la Lebanon.
Amehimizia heshima ya uhuru wa nchi hiyo na utekelezaji kamili wa Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 1701, ambalo linalenga kuzuia makundi yasiyo ya serikali kufanya shughuli za kijeshi nje ya mamlaka ya nchi kusini mwa Lebanon.
“Watu wa Lebanon pamoja na Waisraeli na watu wengine wote katika kanda hii wanastahili kuishi bila hofu,” amesema. “Ili watoto wao wakue bila sauti za ving’ora na mashambulizi, na kurudi nyumbani bila kujua lini watakimbia tena.”