“Wafanyakazi wa afya wako mstari wa mbele kuokoa maisha, na mashambulizi kama haya hayakubaliki,” amesema msemaji wa WHO katika taarifa iliytolewa leo kupitia mtandao wa kijamii wa shirika hilo wa X.

Limeongeza kuwa “Wafanyakazi wa huduma za afya na vituo vya afya lazima walindwe kila wakati chini ya sheria za kibinadamu za kimataifa. Hawapaswi kushambuliwa au kutumika kwa shughuli za kijeshi.”

Mashambulizi Yalenga Huduma za Afya

Madaktari 12, watoa huduma na wauguzi wameuawa katika shambulio usiku wa Ijumaa katika kituo cha afya cha msingi cha Bourj Qalaouiyeh.

Saa chache kabla ya hapo, wahudumu wawili waliuawa katika mashambulizi dhidi ya kituo cha afya huko Al Sowana.

“Tukio hili linaonesha mashambulizi yanayoendelea dhidi ya mfumo wa afya wa Lebanon, ambao ni muhimu kwa wananchi wanaohudumiwa,” ilisema taarifa ya WHO. “Tangu Machi 2, tumehakiki mashambulizi 27 dhidi ya vituo vya afya nchini Lebanon, yakiwemo vifo 30 na majeruhi 35.”

Hatari zinazoongezeka kanda zote

Shirika hilo limeonya kuwa kuongezeka kwa mzozo nchini Lebanon na Mashariki ya Kati kwa ujumla kunaongeza uwezekano wa matukio kama haya.

“Hatua za dharura zinahitajika kupunguza mvutano na kulinda afya ya watu katika kanda hii,” limesema shirika la WHO.

“Hii si tu hasara kwa Lebanon; ni hasara kwa ubinadamu,” ameongeza msemaji wa WHO. “Tunahitaji kuchukua hatua sasa kulinda wahidumu wa afya na kuhakikisha raia wanaweza kupata huduma za afya wakati huu wa mgogoro unaoongezeka.”

Wito wa kulinda huduma za afya

WHO imewataka wahusika wote wa mzozo kuheshimu huduma za afya. “Mashambulizi dhidi ya madaktari, wauguzi, na vituo vya afya yanapingana na kanuni za msingi za ubinadamu,” ilimesisitiza shirika hilo. “Tunashauri hatua za haraka kulinda maisha na kuzuia hasara zaidi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *