#HABARI: Mbunge wa Jimbo la Segerea (CHAUMMA), Mhe. Agnesta Kaiza, ametembelea Kituo cha Watoto Yatima cha Mwana Orphanage jijini Dar es Salaam, na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali yakiwemo chakula, vifaa vya shule, na fedha taslimu kiasi cha shilingi laki mbili.

Mhe. Kaiza amepongeza uongozi wa kituo hicho kilichopo Vingunguti kwa malezi bora wanayoyatoa, akibainisha kuwa msaada huo ni mkono wa heri kuelekea sikukuu za Iddi na Pasaka kwa watoto hao wenye uhitaji.

Msimamizi wa kituo hicho, Bi. Sada Omary Ally, amemshukuru Mbunge huyo kwa msaada wake lakini akaibua kilio cha dhuluma ya nyumba waliyokuwa wakiishi watoto hao awali, jambo linalowalazimu kulipa kodi ya laki tano kila mwezi.

Bi. Sada amemuomba Mhe. Kaiza kuwasaidia kupata haki yao ili kuepukana na mzigo huo wa kodi ambao ni mkubwa kwa kituo, huku watoto wakiongozwa na Naifat Nassor wakieleza matumaini yao ya kupata utatuzi wa changamoto hiyo ya makazi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *