#MICHEZO: Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Mbwana Samatta, ametangaza rasmi kustaafu kuichezea timu hiyo kuanzia Julai 7, 2026.
Kupitia taarifa aliyoitoa nyota huyo anayekiwasha Le Havre ya Ufaransa amesema miaka 15 aliyoitumikia timu hiyo na miaka 10 ya kuwaongoza wenzake kama nahodha, inatosha, na sasa ni wakati wa kutoa nafasi kwa vipaji vipya.
“Naamini huu ni wakati wa vipaji vipya kupewa nafasi ya kutufikisha kwenye hatua za juu zaidi”.
Katika taarifa hiyo, Samatta pia amewashukuru wadau wote wa soka wakiwemo mashabiki, familia yake, TFF pamoja na Serikali ya Tanzania.
Hata hivyo, Samatta ameahidi kuendelea kutoa mchango wake kwa timu hiyo kupitia maeneo mengine ambayo yako ndani ya uwezo na uzoefu wake.
Kwa taarifa zaidi ufuate (follow) ukurasa wetu mpya wa Facebook #ITV EXTRA>>>> https://www.facebook.com/share/1QMjXDHqGv/?mibextid=wwXIfr
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
Follow ITV TANZANIA RadioOne Tanzania

(Feed generated with FetchRSS)