Ingawa haijulikani mahali alipo, azma yake iko wazi, chama cha kiongozi huyo wa upinzani kinasema. Kiongozi wa upinzani wa Uganda Bobi Wine, ambaye alikuwa akiishi mafichoni kwa miezi miwili kufuatia uchaguzi uliopingwa wa mwezi Januari mwaka huu, sasa yuko nje ya nchi. Alitangaza hili mnamo Machi 14.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na chama chake, kiongozi wa National Unity Platform (NUP) aliondoka nchini huku kukiwa na mvutano mkubwa. Makao yake yalikuwa yamezingirwa na vikosi vya usalama. NUP sasa inatetea kuondoka kwake.

Upinzani wa Uganda unasema, kuondoka kwa Bobi Wine si kutaka hifadhi ya kisiasa. Kulingana na wasaidizi wake, ni mkakati wa muda: kiongozi wa National Unity Platform (NUP) anatarajiwa kufanya mashauriano na wanasiasa walio nje ya nchi na wanachama wa diaspora wa Uganda.

Joel Ssenyonyi, msemaji wa NUP, amemwambia Christina Okello: “Kuondoka nchini kimsingi ni kukutana na jumuiya ya kimataifa na viongozi wengine, ili kuona jinsi ya kutoa shinikizo zaidi kwa utawala huu katika ngazi zote.”

Wasaidizi wake wanafananisha tukio hili na lile la kihisoria la Rais Yoweri Museveni mwenyewe, ambaye aliishi mafichoni miaka ya 1980 kwa msaada wa raia. Kulingana na upinzani, Bobi Wine pia aliweza kjkaa mafichoni kwa wiki kadhaa kwa msaada wa wafuasi wake.

Mahali alipo hapajulikani

Licha ya kutokuwepo kwa kiongozi wake, chama cha National Unity Platform (NUP) kinabainisha kwamba upinzani unaendelea kufanya kazi. “Faida ni kwamba, baada ya muda, tumeweka miundo na mifumo mahali pake,” ameongeza Joel Ssenyonyi. “Kwa hivyo, hata anapokuwa hayupo, chama kinaendelea kufanya kazi, kazi inaendelea.” Hapo awali, mara nyingi alikuwa akisafiri kwa ajili ya shughuli, wakati mwingine akiwa mbali kwa wiki moja au mbili kukutana na jumuiya ya kimataifa. Na bado, chama kiliendelea kufanya kazi. Unapokuwa umejenga miundo imara baada ya muda, hakuna mapengo. Hiyo ndiyo hali ya leo”.

Kwa sababu za usalama, eneo halisi la Bobi Wine halijawekwa wazi. Kulingana na wasaidizi wake, shughuli zake katika ngazi ya kimataifa zinaweza kudumu wiki kadhaa kabla ya kurejea nchini Uganda.

Bobi Wine, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, 44, alikimbilia mafichoni siku moja baada ya uchaguzi wa urais wa Januari 15, 2026. Akikosolewa na waangalizi na mashirika yasiyo ya kiserikali, Yoweri Museveni, 81, ambaye ametawala Uganda kwa mkono wa chuma tangu 1986, aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.

Mtoto wa mkuu wa nchi na mkuu wa jeshi wa Uganda, 51, anayejulikana kwa machapisho yake yenye utata kwenye mitandao ya kijamii, aliandika kwenyemtandao wa kijami wa X kwamba alitaka Bobi Wine auawe, ujumbe ambao ameufuta tangu wakati huo. Muhoozi Kainerugaba alipongeza vifo vya wanachama 30 wa upinzani na kukamatwa kwa wafuasi wao wapatao 2,000 kufuatia uchaguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *