Askari watatu wa Senegal wamefariki na wengine watatu wamejeruhiwa siku ya Jumanne asubuhi, Machi 17, katika ajali wakati wa operesheni za kuharibu mashamba ya bangi huko Casamance, karibu na mpaka wa Gambia. Operesheni hizi zimekuwa zikiendelea kwa zaidi ya wiki moja.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff

Katika taarifa, jeshi la Senegal halikutoa taarifa iliyo wazi kuhusu mazingira ya tukio hilo. Kulingana na vyanzo kadhaa, wanajeshi hao watatu walifariki wakati moja ya makombora yao yalipopata joto kupita kiasi na kulipuka walipokuwa wakishiriki rasmi katika operesheni ya kuharibu shamba moja la bangi.

Hata hivyo, chanzo cha kuaminika kilisema kwamba “matumizi ya urushaji wa makombora yanaonyesha wazi kwamba kulitokea makabiliano,” kikielezea kwamba jeshi kwa kawaida hufyatua risasi kwanza ili kuondoa makundi yoyote yenye silaha kabla ya kuendelea kuharibu mashamba hayo.

Operesheni zinaendelea kwa zaidi ya wiki moja

Kwa zaidi ya wiki moja, jeshi la Senegal limekuwa likifanya operesheni kubwa kaskazini mwa Sindian, haswa katika maeneo ya Djiakine, Ifanga, na Kadialock, katika eneo la Bignona, karibu na mpaka wa Gambia. Operesheni hizi zinalenga kuharibu mashamba ya bangi na pia “kuwaangamiza” watu wenye silaha wanaolima bangi, ingawa hakuna takwimu kamili za majeruhi zilizotolewa katika hatua hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *