#HABARI: Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Kilimanjaro limemkamata Emmanuel Kawiche, dereva wa gari la shule, akiwa anaendesha wanafunzi akiwa katika hali ya ulevi mkubwa.

Kamanda wa Polisi wa kikosi hicho mkoani humo, ACP Nassor Sisiwaya, amebainisha kuwa kukamatwa kwa dereva huyo ni matokeo ya operesheni maalumu ya ukaguzi wa magari na upimaji wa kilevi kwa madereva inayolenga kudhibiti ajali na kulinda maisha ya watoto barabarani.

Dereva huyo amekiri kosa la kunywa pombe kabla ya kuanza safari na kuomba radhi kwa kitendo hicho kilichofanyika ndani ya Manispaa ya Moshi.

Wakati huohuo baadhi ya wananchi wakipongeza juhudi hizo za jeshi la polisi, ACP Sisiwaya amesisitiza kuwa wamejipanga vyema kuimarisha ulinzi na ukaguzi zaidi katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ili kukomesha uzembe wa madereva unaohatarisha usalama wa raia na mali zao.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *