Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali haina budi kikusanya kodi kwani nchi haiwezi kuendelea bila fedha.
Kwa mujibu wa Rais Samia, hatuwezi kufanya chochote kama kodi haitokusanya ikiwamo shughuli za maendeleo na kutatua kero za wananchi.
Rais Samia ambaye alikuwa akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kupokea ripoti ya Tume ya Rais ya Kutathmini Maboresho ya Mfumo wa Kodi nchini, Ikulu Jijini Dar es Salaam Machi 18, 2026 amewashukuru wananchi na wafanyabiashara wanaolipa kodi kwa hiari
“Niwapongeze pia wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla kwa moyo wa uzalendo wa kuendelea kuliipa kodi kwa hiari bila shuruti ingawa bado kuna wakwepaji lakini wengi wakishikwa hivi wanalipa kwa hiari bila shuruti. Asanteni sana kwa kuunda juhudi za Serikali,'” amesisitiza
(Feed generated with FetchRSS)