Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Makamu Rais wa pili wa Bunge la Seneti Bahati Lukwebo, ametangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake baada ya kuanzishwa kwa mchakato wakutaka kumuondoa kwenye nafasi hiyo kwa kile Maseneta wanasema hawana imani naye.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kujiuzulu kwa Lukwebo, kumekuja wakati tume ya ukaguzi wa saini ya kutokuwa na imani naye lilianza kukagua zahidi ya saini 80 ili aweze kutimuliwa kwenye wadhifa huo, baada baadhi ya Maseneta kukosoa utendakazi wake. Clément Muboyayi ni seneta aliye saini ombi hilo

Hatukumlazimisha Naibu Speaker wa pili kujiuzulu, lakini alijifanya mjanja na alikuwa makini, na kwa heshima alichagua kujiuzulu badala ya kuendelea kukabiliana na maseneta walio saini maoni yakutokuwa na imani naye. Kujiuzulu kwake kutafungua njia kwa uchaguzi. Ni awamu mpya lingine.”

Hata hivyo, wana chama cha AFDC-A chama cha Lukwebo, waendelea kusema kuwa, hii niulipizaji kisasi kwa namna la kisiasa. Philippe Udji ni Naibu Katibu wa chama cha Lukwebo AFDC-A.

Huu ni uamuzi wa kisiasa ambao yeye kama kiongozi wa chama kisheria, amekubali. Ili kuweka kipaumbele kwa umakini wa taasisi kwenye vita vinavyo endelea Mashariki, tumeamua kwamba Raïs na mamlaka ya maadili lazima wawasilishe kujiuzulu kwake.”

Wiki iliyo pita, mbele ya vyombo vya habari, Lukwebo alipinga mradi yoyote wa marekebisho ao mabadiriko ya Katiba. Msimamo huu ulionekana kama “usaliti” ndani ya familia yake ya kisiasa, Union Sacrée vyama vinavyo msapoti raïs Tshisekedi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *