Wakimbizi wa ndani kutoka majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini waliokimbilia mjini Lubumbashi, kwa sababu ya utovu wa usalama Mashariki mwa DRC, wanalalamikia hali ngumu ya maisha ambapo wanakosa misaada muhimu ya kibinadamu, ambapo siku ya Jumatano waliandamana na kuomba msaada.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwenye lango la kuingilia ofisi ya mkuu wa mkoa Jumatano asubuhi, mamia ya wakimbizi wakiwemo wanawake na watoto walikuwa wameketi chini. Wengine, wakionekana kuwa wamechoka na wenye njaa, wamelala chini. Nao wanaomba msaada,” alieleza kiongozi wao Paul Byamungu.

“Hatuna mahali pa kulala, hatuna chakula, na hatuna huduma ya afya. Nyumba ndogo zilizotuhifadhi, zilianguka kufuatia mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni. Takriban familia zote zinalala nje usiku kucha. Tumekuja hapa kuona mamlaka ili ziweze kutusaidia.”

Bibi Destinée Riziki ni mkimbizi toka muji Bukavu

“Tanaomba vyongozi watizame jambo hili , tupate mahali pa kuhidhazi mfano wa kambi la wakimbizi. Tunateseka sana.”

Kwa wiki kadhaa, wahami hao wanalalamika kwa vyongozi mbali mbali wa mkoa bila mafanikio. Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa haki za binadamu IRDH, Hubert Tshiswaka anasikitika

“Wahami hawa walilala njee usiku kucha. Tunasikitika kuona vyongozi wetu wanawachilia raia, wanausika tuu na shugui zingine. Jambo hili linatuuzunisha sana.”

Baadhi ya vyanzo usema kuwa Kinshasa inatenga fedha za kila mwezi kwa wizara ya maswala ya kibinadamu ya jimbo kusaidia wakimbizi wa ndani. Lakini Valérienne Mumba, waziri wa mkoa wa masuala ya kibinadamu, anasema anasubiri uamuzi wa gavana kabla ya kuchukua hatua. Hata hivyo, wakimbizi hao bado wanaendelea kuketi mbele ya ofisi ya mkoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *