
Bei ya gesi barani Ulaya imepanda kwa 35% siku ya Alhamisi kufuatia mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nishati katika Mashariki ya Kati, na hasa shambulio la Iran linalolenga kituo kikubwa zaidi cha uzalishaji wa gesi asilia iliyoyeyushwa duniani huko Qatar.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Muda mfupi baada ya biashara kufunguliwa saa 7:00 asubuhi, mkataba wa hatima wa Uholanzi TTF, unaochukuliwa kuwa kipimo cha Ulaya, ulipanda kwa 24.13% hadi euro 67.85 kwa kila megawati kxa saa, baada ya kupanda hadi 35%.
Bei ya mafuta pia imepanda leo Alhamisi, pia ikitegemea maendeleo katika mzozo wa Mashariki ya Kati, huku mafuta ghafi ya Brent yakipanda kwa zaidi ya 5%.
Shambulio la ndege isiyo na rubani liligonga moja ya viwanda vikubwa zaidi vya kusafisha mafuta vya kampuni ya mafuta ya Kuwait leo Alhamisi asubuhi, na kusababisha moto katika moja ya vitengo vyake, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.