Picha za setilaiti za NASA zinaonyesha moto mkubwa uliotokea katika kituo kikubwa zaidi cha kuzalisha gesi duniani huko Qatar.

Data za setalaiti kutoka kwenye mfumo wa NASA FIRMS zinaonyesha kwamba maeneo kadhaa ya kiwanda cha kusafishia gesi cha Ras Laffan huko Qatar yameteketea kwa moto baada ya mashambulizi ya jana usiku ya Iran. Picha hizo za satalaiti inayofuatilia mabadiliko ya joto, zinathibitisha kwamba sehemu za kituo hicho cha kimkakati zinateketea kwa moto.

Kiwanda hicho cha kusafishia gesi kilishambuliwa jana usiku kufuatia shambulio la utawala wa kihalifu wa Israel kwa msaada wa Marekani dhidi ya sehemu ya mtambo wa gesi wa Iran, kusini mwa nchi.

Kama mojawapo ya vituo muhimu zaidi vya gesi duniani, Ras Laffan ina jukumu muhimu katika kusambaza nishati kwenye masoko ya kimataifa, na dosari yoyote katika shughuli zake unaweza kuwa na athari kubwa za kiuchumi kwa kanda na dunia.

Iran ilikuwa imetahadharisha kwamba shambulizi lolote la Marekani na Israel dhidi ya taasisi zake za mafuta na gesi litajibiwa papo hapo kwa kushambuliwa taasisi za gesi na mafuta za Mashariki ya Kati zinazomilikiwa na makampuni ya Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *