Kulingana na shirika hilo mpaka umefunguliwa pande zote mbili, lakini ni kwa ajili ya ” Kuruhusu idadi ndogo ya watu kuondoka kutoka eneo la Palestina kwa madhumuni ya kuhamishwa kisaikolojia na kiafya, pamoja na “kurudi kwa idadi sawa ya watu Gaza.”

Hata hivyo, ufunguzi huu wa sehemu, ingawa ni muhimu, bado haujafikia mahitaji ya kibinadamu yanayokolea ardhini.

“Kama tulivyoeleza mara kwa mara, mpaka huu lazima ufunguliwe kwa ufanisi ili kuruhusu uhuru wa harakati za watu wanaoingia na kutoka Gaza na kurahisisha utoaji wa misaada ya kibinadamu na bidhaa,” amesema Olga Cherevko, msemaji wa OCHA, akizungumza na UN News,  na kubainisha kuwa mgogoro wa kibinadamu Gaza unabaki “kuwa mkubwa zaidi na hali za maisha za wananchi bado ni hatarishi.”

Gari la Umoja wa Mataifa linajitayarisha kusafirisha wagonjwa kutoka Hospitali ya Al-Amal huko Rafah, Gaza, inayoshirikiana na Jumuiya ya Palestina ya Mwezi Mwekundu, wakati watu wanakusanyika.

Gari la Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), ambalo linasimamia usafirishaji wa wagonjwa hadi kuvuka mpaka wa Rafah siku ya kwanza ya kufunguliwa tena (Maktaba)

Vifaa vya matibabu na misaada viko chini ya vikwazo

Katika muktadha huu, wahusika wa kibinadamu wanasisitiza kwamba vikwazo vya uendeshaji vinaendelea licha ya ufunguzi huu mdogo.

Mashirika ya misaada bado yanakumbana na “vikwazo vingi vinavyowazuia kutoa msaada na huduma kwa watu wanaohitaji.”

OCHA inabainisha kuwa “vikwazo vikali vilivyowekwa kwa bidhaa ambazo mamlaka ya Israel inaziona zina matumizi mara mbili. Hizi ni pamoja na bidhaa kama kuni, zana za ukarabati wa makazi, saruji, vifaa vizito vinavyotumika kuondoa vifusi na miundombinu iliyoharibika, kutoa nafasi zaidi na kutoa makazi bora, pamoja na vifaa vingi vya matibabu”.

Wakati huo huo, vikwazo hivi vinaathiri moja kwa moja huduma muhimu, hasa katika sekta ya afya.

OCHA inasema takriban asilimia 40 tu ya vituo vya afya ndivyo vinafanya kazi, na wengi wao wanafanya kazi kwa sehemu tu.

Umoja wa Mataifa, unasisitiza vikwazo hivi lazima viondolewe. “Lazima tuweze kupata ufikiaji wa haraka, salama, endelevu na usiokatizwa ili kutoa misaada kwa kiwango kikubwa na kuharakisha juhudi zetu,” amesisitiza Bi. Cherevko.

Zaidi ya watu 11,000 wasaidiwa ndani ya wiki moja

Wakati huo huo, operesheni za kibinadamu zinaendelea licha ya rasilimali na vifaa vilivyopunguzwa.

Katika wiki iliyopita, washirika wa makazi wametoa msaada kwa familia zaidi ya 2,200  ambapo ni jumla ya watu zaidi ya 11,000 kote Gaza. Vifaa hivi vilijumuisha vifaa vya dharura vya makazi ikiwa ni pamoja na kamba, vipimo, sufuria, vyungu, na sahani.

Hata hivyo, wahusika wa kibinadamu wameripoti kwamba vifaa kama mahema, vitanda na vifaa vingine muhimu vinaisha haraka. Baadhi ya washirika wamelazimika kununua kwenye soko la ndani kile wanachoweza kama nguo, vitanda, na vifaa vya msingi vya kupikia moja kwa moja kutoka kwa wauzaji ambao tayari uwezo wao umekwisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *