
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, ametoa onyo kuhusu uhalifu wa Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran, akisisitiza kuwa moto wa mgogoro huu unaweza kuenea na kuwaathiri wengi.
Kwa mujibu wa ripoti ya shirika rasmi la habari la Iran, IRNA , alfajiri ya Ijumaa, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameandika katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii X kwamba: “Asili ya utawala wa Kizayuni imejengwa juu ya ugaidi wa kiserikali. Hata hivyo, kile kilichotokea katika uvamizi wa Marekani dhidi ya Iran na mauaji ya kigaidi ya kiongozi shahidi ni mweleko mpya katika migogoro ya kimataifa ambao unaweza kuvunja misingi ya mifumo ya sheria ya kimataifa.”
Rais Pezeshkian amesisitiza kwamba ikiwa jumuiya ya kimataifa haitasimama kwa msimamo thabiti kukabiliana na mgogoro huu, basi moto wa mzozo huu utaenea na kuwagusa watu na mataifa mengi.
Siku ya Alhamisi pia, Rais Pezeshkian alituma ujumbe na kuandika kuwa: Mashambulizi dhidi ya miundo msingi ya nishati ya Iran yana taathira ambazo ukubwa wake utaitatiza dunia nzima.
Alindika katika mtandao wa kijamii wa X kwamba: Ninalaani vikali mashambulizi dhidi ya miundo mbinu ya nishati ya Iran.
Hatua za kichokozi kama hizi hazitakuwa na manufaa kwa audi Mzayuni, Marekani na waungaji mkono wao bali zitaifanya hali ya mambo kuwa mbaya zaidi na kusababisha taathira zisizoweza kudhibitiwa zinazoweza kuiyumbisha dunia nzima.
Mapema Jumatano Israel na Marekani zilishambulia baadhi ya maeneo ya visima vya gesi vya Pars-Kusini vinavyopatikana kusini mwa Iran katika siku ya 19 ya vita vilivyoanzishwa na tawala mbili hizo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Iran imejibu uchokozi huo kwa kuchambulia vituo vikubwa zaidi vya kusalisha gesi katika nchi za Saudi Arabia na Qatar ambavyo vinamilikiwa na makampuni ya Marekani.