Maafisa wa serikali ya Marekani wamegundua ndege zisizo na rubani zisizojulikana juu ya kambi ya kijeshi huko Washington ambako Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Vita wa Marekani wanaishi.

Gazeti la Marekani, Washington Post, limeripoti kwamba ndege zisizo na rubani zisizojulikana zimeonekana zikiruka juu ya makazi ya Marco Rubio na Pete Hegseth, na kwa mujibu wa vyanzo vyenye taarifa, mamlaka bado hazijabaini ndege hizo zisizo na rubani zimetokea wapi.

Ndege zisizo na rubani zilizokuwa zikiruka juu ya kambi ya kijeshi ya McNair zimewalazimisha mafisa wa serikali ya Marekani kuchunguza suala la kuhamisha makazi ya Rubio na Hegseth.

Hata hivyo, afisa mkuu wa serikali amesisitiza kwamba mawaziri hao wawili bado hawajahamishiwa eneo lingine.

Itakumbukwa kuwa mnamo Februari 28 utawala wa Kizayuni wa Israel na jeshi la Marekani walifanya shambulio la pamoja la anga dhidi ya Iran kumuua shahidi Kiongozi Mkuu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, na makamanda kadhaa wakuu wa jeshi la Iran.

Ripoti zinasema, jeshi la Marekani linafuatilia kwa karibu zaidi vitisho tarajiwa kutokana na kiwango cha tahadhari kinachoongezeka kwa sababu ya vita vya nchi hiyo na Israel dhidi ya Iran.

Pentagon na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani hazijatoa maoni yoyote kuhusu ndege hizo zisizo na rubani zilizoonekana juu ya makazi ya mawaziri wa mambo ya nje na vita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *